Katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Sayyid Ja‘far Musawīzādeh, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa tabligh wa Kimataifa wa Hawza, ameuelezea ujumbe wa hivi karibuni wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa mia moja tangia kuasisiwa upya kwa Hawza ya Qom kuwa ni “katiba ya kihistoria kwa Hawza,” na kwa kusisitiza maudhui yenye thamani ya ujumbe huo, amesema: Ushauri muhimu zaidi uliotolewa na Kiongozi Mkuu katika katiba hiyo tukufu ni kuzingatia fursa zisizokuwa na kifani ambazo ziko mbele ya taasisi za kidini katika ulingo wa kimataifa.
Akinukuu sehemu ya mwanzo ya katiba hiyo, aliongeza kuwa: Kiongozi wa Mapinduzi, kwa mtazamo wa kihistoria, ameelezea hali ya kisiasa iliyogubikwa na ukandamizaji huko Iraq na mataifa mengine wakati wa kuasisiwa kwa Hawza ya Qom na Ayatollah al-Udhma Sheikh Abdulkarīm Hā’irī Yazdī (ra). Kiongozi Mkuu amesisitiza kuwa kuanzishwa kwa Hawza katika mazingira hayo ya kiza ilikuwa ni ishara ya mapambano na hekima ya maulamaa.
Mkurugenzi wa tabligh wa Kimataifa wa Hawza alisisitiza kuwa: Leo hii, kwa kuwepo kwa walinganiaji wa dini wanaofanya kazi katika lugha mbalimbali kwenye maeneo tofauti duniani ni fursa ya kipekee kwa ajili ya kusambaza maarifa ya Kiislamu imejitokeza, fursa hii ya kihistoria kamwe haifai kupuuzwa.
Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Musawīzādeh, sambamba na hilo alitahadharisha juu ya vitisho vya maadui, akasema: Maadui kwa njia ya daima na kwa kutumia nyenzo mpya za mawasiliano, wanajitahidi kuizima “Nuru ya Mwenyezi Mungu.” Vitisho hivi haviwezi kufumbiwa macho.
Ameeleza kuwa miongoni mwa sababu muhimu za kuifanya Hawza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuenea kimataifa ni kwenda sambamba na zama na kushirikiana kwa njia chanya na taasisi za kimataifa. Amesema: Kusawazisha taaluma na mahitaji ya sasa, kutumia mbinu mpya za tabligh na zenye ufanisi, kuanzisha mawasiliano yenye kuleta matunda na taasisi za kimataifa, pamoja na kuimarisha uhusiano wa karibu na taasisi za kidini hasa katika dini mbalimbali kama Ukristo, ni miongoni mwa sababu za mafanikio katika kuifikisha Hawza kwenye kiwango cha kimataifa. Mwingiliano huu wa kidini unaweza kuwa na manufaa makubwa na kuleta athari za dhahiri.
Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Musawīzādeh pia amesisitiza juu ya umuhimu wa pekee wa mawasiliano kati ya wanazuoni wa Kiislamu na vijana katika uwanja wa kimataifa, akasema: Vijana ndio watu muhimu zaidi katika kupokea mafundisho safi ya kimungu. Kijana ni mche wa mti ambao kwa kutunzwa, hugeuka kuwa mti mkubwa na wenye mizizi, matunda ya mti huo yatakuwa na athari kubwa.
Mkurugenzi huyo pia amegusia tofauti ya vizazi na kusema: Mawasiliano ya wanafunzi wa dini (tullab) na vijana yanapaswa kuwa ya karibu mno na tofauti kabisa na mbinu za vizazi vilivyopita.
Amehitimisha kwa kusisitiza ulazima wa kutumia mbinu na nyenzo za kisasa ili kufanikisha mawasiliano haya kwa ufanisi: Iwapo tunataka kufanikisha mawasiliano haya, ni lazima tutumie nyenzo na mbinu za kisasa.
Maoni yako